Kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na timu ya Chuo Kikuu cha Pretoria, inayofahamika kama Tuks FC ya Afrika Kusini ambayo inashiriki katika Ligi Daraja la Kwanza.
Timu hiyo yenye maskani yake Hatfield mjini Pretoria imekuwa ikisajili wachezaji wazoefu katika siku za hivi karibuni ili kupambana kurejea katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Dida ametua kikosini hapo akitokea Yanga ambapo amemaliza mkataba wake na ameondoka akiwa mchezaji huru.
Akitumia ukurasa wake wa Instagram, Dida amepost picha na kuandika ALWAYS BELIEVE.
Kabla ya kufika hapo, Dida amewahi kuwa kipa wa Manyema FC, Simba, Azam FC, Mtibwa Sugar na Yanga.
0 comments :
Post a Comment