Hivi karibuni ilitoka taarifa ya klabu ya Ndanda kumsajili kiungo Athumani Idd ‘Chuji’ na mchezaji huyo akathibitisha kupitia Clouds FM kwamba tayari amemalizana na timu hiyo ya Mtwara.
Baadae zikaja taarifa nyingine kwamba Chuji amekataliwa na Ndanda kutokana nanmgongano wa kiungozi ndani ya klabu hiyo ambao kwa sasa umemalizwa.
Nestory Chilumba ni kaimu mkurugenzi wa Ndanda na yeye ndio alimsainisha mkataba Chuji wa kuitumikia Ndanda. Ametoa ufafanuzi kuhusi kuhusu utata ulioibuka baada ya usajili wa Chuji.
“Kwanza ni kweli tulimsaini Chuji kwa mkataba wa mwaka mmoja, mimi ndio nilimsainisha na akaenda hadi Mtwara kuungana na timu.”
“Kutokana na sababu za kifamilia ambapo alipata taarifa kwa mama yake ni mgonjwa na hawezi kuitumikia klabu ya Ndanda akiwa Mtwara mbali na mama yake, akatuomba kuondoka akajiunge na Coatal Union.”
“Tulimruhusu aende akaitumikie klabu ya Coastal Union lakini alipata baraka za benchi la ufundi.”
“Sasa hivi Chuji sio mvhezaji wa Ndanda, ni mhezaji wa Coastal Union na alipewa hiyo ruhusa na uongozi.”* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment