Msanii wa Bongo Fleva, Chid Benz amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema Chid Benz amekamatwa na watuhumiwa wengine saba kufuatia msako mkali uliofanyika Agosti 12 majira ya jioni.
Akifafanua zaidi Kamanda Hamduni alisema: “Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha Msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa.”
Chid Benz ambaye kwa sasa anafanya vizuri kupitia wimbo wake wa ‘Muda’ aliyomshirikisha Q Chillah si mara ya kwanza kukutwa na tuhuma kama hizo kwani alishawahi kukamatwa na dawa za kulevya aina bangi mkoani Mbeya.
Miezi ya hivi karibuni msanii huyo alikiri kutumia madawa ya kulevya na mara kadhaa alipelekwa kwenye vituo vya kumsaidia kuacha kutumia madawa hayo na alipotoka alisema yuko fiti kiafya lakini baada ya muda imekuwa ikidaiwa anarejea kwenye matumizi yaleyale ya madawa.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment