NA WINFRIDA MTOI
KIUNGO wa timu ya soka ya Simba, Said Ndemla, anatarajia kuondoka Ijumaa wiki hii kuelekea nchini Sweden ambako atafanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya AFC Eskilstuna.
Ndemla ataondoka sambamba na straika chipukizi wa timu hiyo kutoka kikosi ‘B’, Moses Vincent, ambapo kama watafanikiwa kufuzu majaribio yao wataungana na Thomas Ulimwengu ambaye anakipiga katika timu hiyo.
Akizungumza na MWANASPORTS LEO jana, wakala wa wachezaji hao, Thomas Nyupi, alisema uongozi wa Simba tayari umetoa ruhusa kwa nyota hao kuondoka.
Alisema Ndemla bado ana mkataba na Simba hivyo kama atafanikiwa kufuzu majaribio atarudi nchini kukaa uongozi ili kuzungumzia dau wanalotaka kutoka kwa AFC Eskilstuna, kwani mchezaji huyo bado ni mali yao.
“Maandalizi ya safari yamekamilika, hivyo Ijumaa ya wiki hii Ndemla pamoja na Vincent wataondoka nchini,” alisema Nyupi.
Nyupi aliongeza kuwa uongozi wa klabu ya AFC Eskilstuna ulivutiwa na wachezaji hao kutokana na kuonyesha kiwango kizuri katika timu zao, hivyo kutaka kuwajaribu ili waweze kujiunga na kikosi chao kinachoshiriki Ligi Kuu ya Sweden


0 comments :
Post a Comment