News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday, 9 August 2017

HEE!! KUMBE USAJILI WA GYAN HAUJA KAMILIKA AONDOKA GHANA BAADA YA SIMBA DAY


Mshambuliaji mpya wa Simba, Nicholas Gyan anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Ghana katika timu yake ya Ebusua Dwarfs ili kukamilisha taratibu za uhamisho wake.
Mchezaji huyo ambaye ametua Simba hivi karibuni na kucheza mchezo mmoja katika kikosi hicho cha Simba, jana Jumanne katika mchezo dhidi ya Rayon Sports, alionyesha kiwango kizuri na kukubalika kwa mashabiki wa Simba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema Gyan alilazimika kuja kushiriki katika mchezo huo wa Tamasha la Simba Day ili atambulike kwa Wanasimba.
Hans Poppe amesema Gyan anamaliza mkataba wake na timu hiyo ya Ghana, Agosti 20, mwaka huu Ebusua Dwarfs na baada ya hapo atarejea nchini kuanza kazi rasmi kujiunga na timu hiyo. 
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment