Wakati presha ya mchezo wa Simba na Yanga ikiendelea kuwa kubwa, Yanga wamemzungumzia mchezaji wao mpya kikosini hapo Papy Kabamba Tshishimbi.
Tshishimbi alitua Dar, juzi akitokea DR Congo ambapo ni nyumbani kwao, kisha moja kwa moja akaelekea Pemba ambapo Yanga imeweka kambi kujiandaa kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya watani wao wa jadi kwa ajili ya kuanza mazoezi.
Akizungumzia mchezaji huyo, Dismass Ten ambaye ni Ofisa Habari wa Yanga, alisema baada ya kutua kiungo huyo anayetajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kukaba ameanza mazoezi lakini alilazimika kufanya mazoezi ya peke yake kwa kuwa wenzake walishaanza mazoezi muda kidogo.
Ten amesema hatua hiyo ya kufanya mazoezi peke yake chini ya uangalizi maalum ni kutokana na kuchelewa kujiunga na wenzake kambini, hivyo atapewa program maalum kwa muda kabla ya kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake.
Kuhusu kucheza au kutocheza katika mchezo ujao dhidi ya Simba, Ten alisema hilo ni suala la mwalimu na benchi lake la ufundi. * USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment