DOZI ZA "4G" ZAANZA KUMTIA KIBURI MOURINHO AMCHEKA CONTE AMWAMBIA ASITAFUTE KISINGIZIO KWA MATIC
JOSE MOURINHO amemtaka kocha wa Chelsea Antonio Conte asitafute visingizio kwa madai ya usajili mbovu msimu huu. Conte amekuwa akilalamikia kumpoteza Nemanja Matic aliyesajiliwa na Manchester United. Lakini Mourinho anafoka: "Unapouza na kununua, tatizo liko wapo hapo? "Tatizo ni pale unapouza halafu ukashindwa kununua. Watu wanasema Chelsea imepoteza kiungo muhimu. Lakini kama umemuuza mchezaji muhimu halafu ukawanunua Bakayoko na Drinkwater kwa mfano, ni lipi tatizo?"
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment