Ikiwa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ilikuwa katika kikao cha kupitisha usajili ambacho kimefikia tamati leo, habari za uhakika kutoka ndani ya TFF zinaeleza kuwa Kiungo wa Yanga, Pius Buswita amefungiwa kuitumikia timu hiyo kutokana na Simba kumwekea pingamizi.
Simba, walimwekea pingamizi Buswita wakidai alisaini katika timu yao kabla ya kusaini Yanga akitokea Mbao FC ya Mwanza.
Ikumbukwe mwishoni mwa mwezi Juni,Simba walitangaza kumsainisha Buswita kabla ya kuibukia Yanga ambayo walimpa mkataba wa miaka miwili.
Mtoa habari huyo alidadavua kuwa kama Yanga watataka kumtumia Buswita basi wamalizane na Simba ambayo fedha walizotanguliza kutaka kumsajili hazijarudishwa.
Hivyo basi, Kamati hiyo kesho itaeleza suala hilo la Buswita ambaye anaweza akakosa katika mchezo wa Jumatano dhidi ya mahasimu wao,Simba.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment