Mkongwe wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs na mkongwe wa zamani wa Liverpool Kenny Danglish walikuwa na rekodi ya kuwahi kubeba vikombe vingi duniani ambapo kila mmoja alikuwa na makombe 35.
Rekodi hii imekuwa ngumu sana kufikiwa na hata wachezaji wakubwa wawili duniani Lioneil Messi na Cristiano Ronaldo wameshindwa kuvunja au kufikia rekodi waliyokuwa nayo Danglish na Giggs.
Ryan Giggs alipata makombe yote hayo akiwa na Manchester United huku Danglish akichukua makombe hayo 14 akiwa na Celtic na 21 yaliyobaki aliyachukua akiwa na klabu yake ya Livepool.
Lakini hapo jana mlinzi wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil Dani Alves alivunja rekodi hiyo ya wakongwe hao wawili baada ya kuisaidia klabu yake hiyo mpya kubeba ubingwa wa French Super Cup.
Alves ameshawahi kushinda kombe 1 akiwa na Bahia, akashinda 3 akiwa na Brazil, akashinda 2 akiwa na Juventus, akashinda 5 akiwa na Sevilla huku akishinda jumla ya makombe 24 akiwa na Barcelona na la jana inamfanya ashinde jumla ya makombe 35.
![](https://is05.ezphotoshare.com/2017/07/17/snRRYI.jpg)
![](https://is02.ezphotoshare.com/2017/07/23/sAYGYx.jpg)
0 comments :
Post a Comment