UGONVI UMEANZIA KUCHUKULIANA MAKOCHA,WAKAJA WACHEZAJI,MAGOLIKIPA SASA KIPUTE UWANJANI hebu pata uhondo hapa..
Timu ya Yanga itacheza mchezo wake wa Kwanza wa Kirafiki kwaajili ya Maandalizi ya Msimu wa 2017/2018 DHIDI ya Singida United.
Ila Mchezo Huu ama kwa hakika utakuwa na Utamu wake Ukianzia Upande wa Makocha ambapo Lwandamina ndiye Aliyechukua Nafasi ya Pluijm hivyo Upinzani Utaanzia Hapo kwa Makocha Hao kutaka Kutambiana nani Mbabe zaidi.
Utamu zaidi Utakuja endapo Golikipa Ally Mustapha Barthez atakuwa Golini upande wa Singida United ama kwa hakika atataka Kuonyesha Yanga kuwa yeye Bado Bora.
Kitu Kingine Itakuwa ni Harakati za Singida United Kutaka Kuonyesha wao na Yanga hawana Undugu kama Wengi wanavyozifananisha Jezi zao,na Viongozi wa Juu wa Singida United kuhusishwa kuwa mashabiki Kindakindaki wa Yanga. Tusubiri 5.8.2017 Uwanja wa Taifa Kushuhudia Mtanange Huo wa Kutest Vikosi.
SHARE HABARI ILI WATU WENGI WAIONE BONYEZA SHARE KWA FACEBOOK HAPO CHINI
0 comments :
Post a Comment