News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday 17 July 2017

TETESI ZA USAJILI JIONI YA LEO 17 JULY 20017: HUKU YAKITIMIA KWA SANCHEZ COSTA AMTUSI CONTE NA MENGINE MENGI...

Tokeo la picha la USAJILI
1.MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Diego Costa amedhidi kumchafua kocha wake Antonio Conte baada ya kuituma video yake Instagram akiwa amevalia jezi ya Atletico Madrid huku akiisindikiza na maneno ya kejeli kwa Lugha ya Kihispaniola, "DALE UN ABRAZO A CONTE" kwa Lugha ya Kiingereza ilikuwa inasomeka kama ,"GIVE A HUG TO CONTE". (#ESPNFC).
2.KIPA WA ARSENAL, Wojciech Szczesny anatarajia kujiunga na mabingwa wa Italia, Juventus kwa ada inayodhaniwa kuwa ni pauni £8m. (#DailyMirror).
3.MSHAMBULIAJI WA CHELSEA Loic Remy anafikiria kuachana na klabu hiyo baada ya kukosa namba ya uhakika katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku vilabu vya Marseille na Everton zikigombea saini yake. (#SkySports).
4.KIUNGO WA CHELSEA Marco Van Ginkel amejiunga rasmi na klabu ya PSV Eindhoven kwa mkopo wa muda mrefu. (#PSV)
5.AC MILAN inataka kujaribu kumchukua Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial kwa mkopo. (#ESPN).
6.KIPA WA MANCHESTER UNITED Sergio Romero ameongeza mkataba mwingine wa miaka minne na klabu hiyo hadi mwaka 2021. (#ESPNFC).
7.BARCELONA imepeleka ofa mpya ya pauni £65m pamoja na Kiungo wao, Ivan Rakitic kwa Paris Saint Germain ili wampate Kiungo wa klabu hiyo, Marco Verratti. (#Calciomercato).
8.MSHAMBULIAJI WA TORINO, Andrea Belloti anataka kujiunga Ac Milan ambao wametoa ofa ya pauni £40m na wachezaji Gabriel Paletta na M'Baye Niang kwa nyota huyo lakini klabu yake ya Torino inataka pauni £100m kwa Muitaliano huyo. (#Calciomercato).
9.ARSENAL imeweka pauni £45m ikitaka kumsajili beki wa Southampton, Virgil Van Dijk. (#DailyExpress).
10.PARIS SAINT GERMAIN imeweka pauni £150m kwa Kiungo Mshambuliaji wa Real Madrid, Marco Asensio ikitaka kumsajili. (#DonBalon).
11.ARSENAL inataka kumsajili Winga Mshambuliaji wa Celtic Moussa Dembele iwapo Mshambuliaji wao, Alexis Sanchez ataondoka klabuni hapo. (#DailyStar).
12.BEKI WA SOUTHAMPTION, Virgil Van Dijk itazipiga chini ofa zote ili aweze kujiunga na Liverpool katika viunga vya Anfield. (#TheSunReport).
13.ARSENAL imerudi Santiago Bernabeu ikitaka kumsajili Mshambuliaji wa klabu hiyo, Alvaro Morata. Kocha Arsene Wenger anaamini Mhispaniola huyo ataziba vilivyo pengo la Sanchez na kuunda safu matata ya Ushambuliaji sambamba na Alexander Lacazette. (#DonBalon).
14.CHELSEA inataka kumsajili Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero lakini klabu hizo hazijaingia kwenye makubaliano na uhamishp huo. (#AsJournalistManuSainz).
15.ARSENAL imemuwekea Mshambuliaji wake Alexis Sanchez ofa ya mshahara wa pauni £275,000 kwa wiki ili kumzuia asiondoke klabuni hapo. (#TheSun).
16.AC MILAN inataka kumsajili Mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata. Tayari klabu hiyo imesajili mastaa Kama Matteo Musachio kutoka Villarreal, Franck Kassie kutoka Atalanta, Leonardo Bonucci kutoka Juventus, Andre Silva kutoka Fc Porto na mastaa wengine. (#LaGazzettadelloSports).
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment