News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday 19 July 2017

SASA LEO NGOMA INARUDIWA ARSENAL MPYA VS BAYERN MAPEMAAA MTU ANAKAA ANGALIA MUDA NA VIKOSI VYA MECHI LEO..


Shanghai, China.

MABINGWA wa kombe la FA nchini England,Arsenal leo mchana mishale ya saa 8:20 watakuwa na kibarua kigumu pale watakaposhuka kwenye uwanja wa michezo wa Shanghai huko Shanghai,China kucheza na Bayern Munich kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa michuano ya International Champions Cup (ICC).

Arsenal inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa jumla ya mabao 10-2 na Bayern Munich kwenye michezo yao miwili ya hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la klabu bingwa Ulaya iliyofanyika Machi mwaka huu.

Katika mchezo wa awali uliochezwa Ujerumani Arsenal ilikubali kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa miamba hao wa Allianz Arsenal na katika mchezo wa marudiano Arsenal ilikubali kichapo kingine cha mabao 5-1 nyumbani Emirates.

Baada ya mchezo wa leo Arsenal itarejea tena dimbani Jumamosi Julai 22 kucheza na Chelsea kwenye mchezo mwingine wa kirafiki utakaochezwa kwenye uwanja wa Bird Nest ulioko Beijing.

 SHARE HABARI ILI WATU WENGI WAIONE BONYEZA SHARE KWA FACEBOOK HAPO CHINI
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment