News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday 19 July 2017

KIUNGO MSHAMBULIAJI ,KIBERENGE AIKACHA LIVERPOOL NA KWENDA.....


Roma,Italia.

KIUNGO Mbrazil,Lucas Leiva amehitimisha safari yake ya miaka kumi ndani ya kikosi cha Liverpool baada ya leo hii kujiunga na Lazio ya Italia kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 5.

Lucas mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na Liverpool mwaka 2007 kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 5 akitokea Gremio ya nyumbani kwao Brazil.

Akiwa na Liverpool,Leiva alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 345,michezo 247 ikiwa ni ya ligi kuu England.Mwaka 2012 Leiva alikuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool kilichotwaa ubingwa wa kombe la ligi.

Lazio imemsajili Leiva ili kuwa mbadala wa moja kwa moja wa kiungo wake Muargentina,Lucas Biglia aliyejiunga na AC Milan juzi Jumapili.

Msimu uliopita Lazio ilimaliza katika nafasi ya tano hivyo kukata tiketi ya kucheza michuano ya Europa Ligi chini ya kocha wake,Simone Inzaghi.

SHARE HABARI ILI WATU WENGI WAIONE BONYEZA SHARE KWA FACEBOOK HAPO CHINI
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment