News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday 9 July 2017

Sanchez ataka Arsenal wamuuze kwa Man City

SANCHEZ

London, England. Alexis Sanchez anataka kujiunga na Manchester City baada ya kuwaambia Arsenal wamuuze sasa.
Nyota huyo wa Chile ametawala katika sakata la uhamisho msimu huu, huku klabu yake za Gunners ikiwa njia panda katika kubakiza akiwa katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake.
Hata hivyo, Manchester City wameonyesha nia ya kutaka kumuogeza Sanchez ndani ya Etihad, ambako atakuwa na kufuraha ya kufanya kazi  pamoja na kocha wake wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola.
Bayern Munich nao walikuwa wakihusishwa na kumtaka nyota msimu huu baada ya kikosi cha Arsene Wenger kushindwa kumaliza katika nne bora.
Lakini gazeti la Chile la El Mercurio limedai kuwa nyota huyo ameamua kubaki England katika klabu ya Man City.
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Sanchez, ameliambia gazeti hili The Sun: “Hakuna mashindani ya Ulaya yaliyokuwa makubwa zaidi ya Ligi ya Mabingwa ndiyo yanayostahili  kucheza Alexis.
“Anapenda kucheza mashindano kama hayo yenye ushindani na kutwaa ubingwa huo.”Sanchez (28), yuko mapumzikoni kwa sasa baada ya kuiongoza Chile kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho la Fifa, ambako mabingwa hao wa Amerika Kusini walifungwa na Ujerumani.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment