
Maswali mengi ambayo yamekuwa Yakiulizwa na Wadau wengi wa Soka Tanzania Na baadhi ya Wakenya Kuhusu Kama Wayne Rooney atakuja Tanzania kwenye Ziara ya Everton kucheza na Gor mahia yamepata Majibu Yake.
Ndugu msomaji wa Msindiforums Kupitia Mtandao rasmi wa Everton Huko Twitter wamethibitisha kuwa Wayne Rooney atakuja Tanzania huku Rooney mwenyewe akisema Ziara ya Tanzania Itakuwa ni nafasi ya kipekee kwa yeye kuwajua Wachezaji wenzake

Rooney amejiunga Na klabu yake ya mwanzo Everton mara baada ya Kuachana na Timu yake ya Manchester United aliyoichezea kwa Miaka Mingi.
0 comments :
Post a Comment