News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday 10 July 2017

RASMI PER MERTESACKER KOCHA ARSENAL BAADA MSIMU HUU WENGER ATHIBITISHA HILO soma habari hio hapa!!


KWA unyenyekevu mkubwa kabisa nahodha wa timu ya Arsenal, Per Mertesacker ameanza kuwaaga mashabiki wa timu hiyo akisema kwamba siku zake za kubaki katika timu hiyo zinahesabika. Nahodha huyo juzi jioni ametangaza kwamba atastahafu mwisho wa msimu wa 2017/18 na kuwa msimamizi wa akademi ya klabu hiyo. Beki huyo alijiunga na Arsenal kutoka Werder Bremen agosti 2011 lakini aliwachezea mechi mbili pekee msimu uliopita kutokana na majeraha. Arsenal wametangaza kwamba wataanza kufanya kazi na Academi ya klabu hiyo kumuandaa kwa jukumu hayo ya baadaye. “Per ni mtu pekee ambaye ni mfano mwema kwa wachezaji chipukizi” meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema. “Hufikiria sana kuhusu mechi na huwa anajitolea kusaidia wachezaji kufikia upeo wao.” Per alirejea kutoka kuuguza jeraha na akasaidia Arsenal kuilaza Chelsea uwanjani Wembley mwezi mei na kutwaa kombe la FA. Per ambaye kwea sasa umri wake umegota miaka 32 alichezea Arsenal zaidi ya mechi 200 na ni mmoja wa wachezaji wanaoheshimika sana katika klabu hiyo. Wenger amesema kwamba Arsenal haiwezi kumuacha mchezaji huyo aondoke moja kwa moja kwani kuna mambo mengine anaweza kufanya kwa ufanisi mkubwa. “Kama kucheza kunaweza kuwa na kikomo lakini huyu simtu wa kumwacha aondoke nadhani anatakiwa kutumikia kwa mambo mengine mengi hapa” amesema Wenger.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment