News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday 12 July 2017

Philippe Coutinho, Vinicius wa Madrid wanusurika kifo uwanjani Brazil

jbbjb

Brazil. Wachezaji Philippe Coutinho wa Liverpool na Vinicius Junior wa Real Madrid anayechezea klabu ya Flamengo ya Brazil, wamenusurika kifo baada ya kuibuka vurugu na kupigwa mabomu ya machozi uwanjani juzi Jumapili.
Kutokana na vurugu hizo, klabu ya Brazil ya Vasco da Gama imeamuriwa kucheza michezo yake bila kushangiliwa baada ya shabiki wake mmoja kupigwa risasi na kufariki dunia baada ya  kundi kubwa kuvamia uwanjani hapo.
Vasco ilifungwa bao 1-0 dihdi ya Flamengo jijini Rio de Janeiro katika mechi  ya watani wa jadi ambao ilikuwa na ushindani mkali.
Mechi hiyo iliyocheza kama fainali ikiwa ni mbio za kusaka taji la ubingwa lakini Flemingo waliibuka na ushindi.
Mchezaji wa Liverpool, Philippe Coutinho ambaye amewahi kuichezea  klabu ya Vasco, naye alikuwapo akishuhudia kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa vurugu kubwa.
Rais wa klabu ya Vasco, Eurico Miranda aliomba radhi kwa wapenzi wa michezo kutokana na taharuki iliyojitokeza.
Shabiki aliyefariki dunia kwenye vurugu hizo alitambulika kwa jina la Davi Rocha (27).
Pia, kinda huyo wa Real Madrid, Vinicius (16) ambaye anachezea Flemengo kwa mkopo wa Pauni 38 milioni aliathirika na mabomu ya machozi na kukimbia uwanjani.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment