News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday 12 July 2017

hiki ndicho kikosi kamili cha wachezaji 25 watakaokuja Tanzania leo hii




Liverpool,England.

NAHODHA wa zamani wa Manchester United,Wayne Rooney ni miongoni mwa wachezaji 25 wa Everton watakaowasili nchini Tanzania leo Asubuhi tayari kwa mchezo wao wa kesho Alhamisi wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa kombe la SportPesa,Gor Mahia ya Kenya maarufu kama K'Ogalo.


Mbali ya Rooney nyota wengine waliojumuishwa kikosini na tayari wameshaanza safari ya kuja nchini ni pamoja na Davy Klaassen,Michael Keane,Leighton Baines na Morgan Schneiderlin.

Kiungo Ross Barkley,mlinzi wa kati Ramiro Funes Mori na mlinda mlango Joel Robles wao wameachwa kutokana na kuwa majeruhi.


Wengine walioachwa ni Mlinda mlango mpya na mchezaji ghali zaidi wa klabu hiyo,Jordan Pickford aliyetokea Sunderland kwa dau la £30m,Mason Holgate na Sandro Ramirez.Hawa wamepewa mapumziko kutokana na hivi karibuni kushiriki michuano ya kombe la Ulaya (Euro) la vijana wenye umri wa chini ya miaka 21.

Kikosi kamili cha Everton kilichoondoka kwenye uwanja wa kimataifa wa Liverpool usiku wa kuamkia leo ni:

Makipa:Maarten Stekelenburg,Mateusz Hewelt,Chris Renshaw. 


Mabeki:Tom Davies,Phil Jagielka,Ashley Williams,Callum Connolly,Jonjoe Kenny,Michael Keane,Muhamed Besic,Leighton Baines.

Viungo:Morgan Schneiderlin,James McCarthy,Davy Klaassen,Gareth Barry,Idrissa Gana Gueye,Joe Williams,Kieran Dowell.

Washambuliaji:Kevin Mirallas,Wayne Rooney,Aaron Lennon Dominic Calvert-Lewin,Ademola Lookman,Matthew Pennington,Yannick Bolasie .

Mchezo kati ya Everton na Gor Mahia utachezwa kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kuanzia mishale ya saa 11:00 za jioni.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment