- Mancheter City wanajaribu kuwapiku Real Madrid katika kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Daily Mirror)
- Manchester City wapo tayari kutoa pauni milioni 160 kumsajili Kylian Mbappe katika harakati za Pep Guardiola kujenga kikosi chake. (ESPN)
- Kylian Mbappe ambaye alipachika mabao 15 katika mechi 29 za Ligue 1 msimu uliopita atakataa kwenda Manchester City akitaka kujiunga na Real Madrid. (Daily Star)
- Manchester City hawajapanda dau lolote kumtaka Kylian Mbappe, na wala hawana mpango huo, ingawa Pep Guardiola amesema Real Madrid hawana ‘msuli’ mkubwa wa kifedha kama wa City. (Sky Sports)
- Real Madrid wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili Kylian Mbappe kwa euro milioni 180. (Marca).
- Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho anakaribia ’sana’ kujiunga na Barcelona (Mundo Deportivo)
- Barcelona wametuma maafisa wake hapa England kujaribu kumsajili Philippe Coutinho, 25, licha ya Liverpool kukataa dau la pauni milioni 72. (Sports)
- Liverpool wanasisitiza kuwa Philippe Coutinho hauzwi, lakini Barcelona wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 80. (Daily Star)
- Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema timu yake haiogopi ‘kumwaga fedha’ msimu huu huku wakiendelea kumsaka beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Daily Mirror)
- Liverpool wanatarajiwa kukamilisha usajili wa Virgil van Dijk kutoka Southampton ifikapo mwisho wa dirisha la usajili. (Sky Sports).
- Arsenal hatimaye wanakaribia kumsajili kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21, kwa pauni milioni 45. (Sun)
- Arsenal wanafikiria kumsajili kiungo wa Nice, Jean Michael Seri. (L’Equipe)
- Arsenal wanakabiliwa na kupata hasara kwa mshambuliaji wake Lucas Perez, baada ya Deportivo La Coruna kutoa pauni milioni 9 kutaka kumsajili mchezaji huyo, 28. (Evening Standard)
- Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anataka kubakia London iwapo ataondoka Emirates, huku West Ham ikionekana ni kimbilio lake. (Independent)
- Stoke City wanataka kununua wachezaji kadhaa katika wiki chache zijazo, lakini hawana mpango wa kumtaka winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23. (Stoke Sentinel).
- Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches, 19, amesema anataka kuondoka Ujerumani huku AC Milan na Manchester United wakimnyatia mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 43. (Independent)
- Tottenham wanafikiria kumsajili beki wa Hoffenheim Jeremy Toljan, 22, baada ya mazungumzo ya kumsajili beki Ricardo Pereira, 23, wa Porto kukwama. (Daily Mail)
- Everton wamepanda dau la pili la pauni milioni 45 kutaka kumsajili kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson. (The Telegraph)
Wednesday, 26 July 2017
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment