News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday, 26 July 2017

MSIKILIZE HIMID MAO AKIELEZEA MIPANGO YA USAJILI WAKE YANGA FC

Himid amasema kwamba kwa sasa anawasiliana na wakala wake ili kujua mustakabali wake wa msimu ujao, kwa sababu kuna ofa nyingi wamepata.
“Tangu wakati nipo Afrika Kusini kwenye COSAFA hizo ofa zilikuwepo, sasa wakala yeye alikuwa anazifanyia kazi, nataraji sasa atakuwa amekwishapata majibu, nitawasiliana naye ili kujua,”alisema mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Himid amesema ana ofa kutoka Misri, Afrika Kusini na Denmark ambako alikwenda kufanya majaribio Aprili mwaka huu, hivyo anasubiri kusikia kutoka kwa wakala wake ili kujua mustakabali wake wa msimu ujao.
Himid Mao anatarajiwa kumaliza mkataba wake Azam FC Novemba mwaka huu na mwenyewe ameonyesha dhamira ya kutotaka kubaki kabisa nchini, licha ya pia kuhusishwa na mpango wa kuhamia kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment