News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Tuesday 18 July 2017

MKWASA AIPA POLE SIMBA SC KWA MATATIZO YA AVEVA, KABURU Soma zaidi hapa


KATIBU mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametoa pole kwa wanachama wa klabu ya Simba kufuatia matatizo yaliyowakumba na kusababisha baadhi ya viongozi wake wa ngazi za juu kufikishwa kwenye vyombo vya dola. Baadhi ya viongozi wa juu wa klabu ya Simba ambao wapo mahabusu ni pamoja na rais wake, Evas Aveva na makamu mwenyekiti Geoffrey Nyange “Kaburu”. “Sisi wote ni familia ya soka hatuwezi kufurahia matatizo yanayowapata viongozi wa Simba wakati huu, suala hili limetugusa na tunawapa pole wanachama wao.” “Hatuna uadui nje ya uwanja, vita yetu ni ya kimpira tu, hivyo yanapotokea matatizo kama haya tunakuwa bega kwa bega katika kufarijiana na kutiana moyo,” alisema Mkwasa. Kesi ya viongozi hao imepangwa kusomwa tena Julai 20, mwaka huu kwenye mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment