Hii iliwahi kutokea lakini haikuandikwa! Sasa sikia, Baada ya PSG kushinda 4-0 dhidi ya Barcelona kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita Meya wa Mont-de-Marsan kule Paris Charles Dayot aliibuka katika ukurasa wake wa Facebook na kuanza kujinadi kwamba kama Barcelona wangeiondoa PSG katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, yeye angekula panya.
Watu walimshangaa kwa kuwa Barcelona ina wachezaji wakali wa kupindua matokeo akiwemo Lionel Messi, lakini yeye aliendelea na msimamo wake. Matokeo yake Barcelona ikafanya maajabu kwa kupindua matokeo na kufanya PSG watoke kwa jumla ya mabao 6-1 kule Uwanjani Camp Nou. Sasa Dayot aliamua kula nyama ya panya ili kumaliza mjadala. Lakini cha ajabu alipomaliza alisema; “Nilikuwa naogopa bure, nyama yenyewe tamu tu, ni kama unakula nyama ya sungura.
0 comments :
Post a Comment