News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday, 10 April 2017

TID AFUNGUKA ANAVYOKERWA NA HELA WANAZO OMBWA NA WATANGAZAJI ILI WAPIGE KAZI ZAO

Msanii wa muziki TID Mnyama amedai anakuchukizwa na baadhi ya wadau wa muziki wanaowadai wasanii pesa ndipo ngoma zao ziweze kuchezwa kwenye vituo vya redio na runinga.
Muimbaji huyo ambaye ameachia video ya wimbo ‘Woman’ wiki iliyopita, alidai wasanii wananyonywa na wadau wanaoshughulika kusukuma muzilki hali amabayo inawafanya wasanii wengi kutenga bajeti ya kufanya matangazo ya kutosha ili kazi ziweze kusikika mitaani na sehemu mbalimbali.

“Nakerwa sana na watu ambao hawajui jinsi gani sisi tunasumbuka. Unalipa studio, video na mambo kibao kwa ajili ya kufanikisha kazi, cha ajabu DJ anaweza akataka kupiga lakini mtangazaji anakwambia acha mpaka atoe kitu huu ni uuaji wa vipaji na ninapigana nao sana,” TID alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV.
Aliongeza,”Sasa wameshatujengea kwenye mindset kuwa ukiandaa ngoma andaa na pesa ya kutulipa ili kazi itembee.,”
Wimbo Woman ni wimbo wake wa kwanza kuutoa toka atoke kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
TID MNYAMA
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment