News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday, 27 March 2017

DJ Sinyorita wa Clouds Fm asema ana mpango wa kuwa mtayarishaji wa muziki


DJ Sinyorita kutoka kipindi cha XXL ya Clouds FM amefunguka kuzungumzua mpango wake mpya wa kuwa mtayarishaji wa muziki nchini.
Akiongea na Gazeti la Mwananchi wiki hii, Dj Sinyorita amedai ataingia darasani ili kujifunza muziki kwa ujumla ile aje kutimiza lengo lake la kuwa mtayarishaji wa muziki.

“Ndiyo nina mpango huo, lakini nikienda sitasoma u-Dj pekee, nafikiria kwenda kusoma muziki kwa ujumla kwa sababu nina mpango wa kuwa mtayarishaji wa muziki,” alisema Sinyorita.
DJ huyo ambaye awali kuwa EATV, amesema haikuwa rahisi kwake kupata nafasi ya kufanya kazi hiyo kwani amepitia changamoto nyingi.
Kwa sasa DJ huyo ndiye DJ pekee wa kile Clouds FM baada ya DJ mkongwe DJ Fetty kuachana na kazi hiyo.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment