News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday, 13 January 2018

WENGER NOMAAAH!! HEBU SOMA HAPA MAJIBU ALIYOWAJIBU MASHABIKI WANAOFIKIRI MWISHO WA MSIMU ATAONDOKA!! KAMA NI MMOJA WAO UTAKAA CHINI ULIE!! teh! teh!!



Licha ya wengi kuamini kuwa Arsene Wenger atatimka Emirates mwishoni wa msimu huu, kocha huyo amesisitiza kuwa atakuwepo Arsenal msimu ujao.

Hatma ya Wenger ipo mashakani baada ya mwendo wa kusuasua msimu huku ikishinda mechi moja tu katika michezo yake sita ya mwisho.

Mfaransa huyo alisaini mkataba wa miaka miwili mwanzoni mwa msimu huu ambapo ndani ya dili hilo, hakuna dau lililowekwa kwaajili ya yeye kuvunja mkataba huo.

Alipoulizwa siku ya Ijumaa iwapo yuko mbioni kutimka Arsenal, kocha huyo alisema: "Nitakuwa hapa msimu ujao, mkataba wangu unadhihirisha hivyo, sijawahi kuvunja mkataba katika historia yangu na sina nia ya kufanya hivyo".
USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment