News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Friday, 1 December 2017

HUU NDIO UKWELI WA KOCHA MKUU SIMBA KAMA AMEONDOLEWA AMA YUPO KAZINI USOME HAPA!!

Tokeo la picha la Joseph Omog
Wakati dirisha dogo la usajili likiwa limefunguliwa tangu Novemba 15, taarifa za usajili katika timu za Simba na Yanga zimeendelelea kusikika kila kukicha.
Habari ya kuwa Simba nayo ipo kwenye mpango wa kumuacha kocha wake, Joseph Omog zimekuwa zikizungumzwa mara kwa mara lakini Ofisa Habari wa SImba, Haji Manara amelizungumzia suala hilo kw amara nyingine.
Alipoulizwa juu ya ukweli wa taarifa hizo, Manara alisema hakuna ukweli juu ya madai hayo na kueleza kuwa kinachozungumzwa ni porojo za mitaani lakini hakuna ukweli halisi kwa kuwa yeye ndiye msemaji wa Simba na kama kungekuwa na ukweli angeweka wazi suala hilo.
“Ni porojo tu za kwenye mitandao, hakuna kitu kama hicho,” alisema Manara.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Simba ilimuondoa Jackson Mayanja aliyekuwa msaidizi wa Omog licha ya kuwa Mayanja mwenyewe alisema ameamua kujiweka pembeni kutokana na masuala ya kifamilia.
Aidha, Manara anatajiwa kuzungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa kwenye makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.

USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment