News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 29 October 2017

PICHA 10 ZA MPAMBANO WA NGUMI KAYI YA JOSHUA vs TAKAM PAMBANO LIMEISHA MUDA MCHACHE ULIOPITA


Bondia Carlos Takam kutoka Ufaransa ambaye alionekana kama sugu hivi, mwisho alishindwa kuvumilia ukali wa makonde ya Anthony Joshua katika raundi ya 10.

Joshua amemshinda Takam katika pambano la uzito wa juu kuwania mkanda wa IBF lililomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Cardiff.

Kabla Joshua alikuwa azichape na Kubrat Pulev lakini aliumia na kujitoa na Takam akachukua nafasi yake.

Ingawa alibezwa na wengi, Mfaransa huyo alionyesha kiwango kizuri na usugu licha ya kwamba Joshua alipiga ngumi nyingi zaidi.

Mabondia hao waligongana vichwa mapema kabisa, lakini walijitahidi kuendelea kupambana hadi raundi ya 10 Takam aliposhindwa.

Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic alionyesha mapenzi yake kwa kumuunga mkono rafiki yake Joshua.

















USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment