
Winga wa kimataifa wa Tanzania anayesakata gozi la ng’ombe kwenye klabu ya Difaa Jadida ya nchini Morocco, Simon Msuva pamoja na mambo mengine ameelezea kuhusu homa ya pambano la Watani wa Jadi, Simba na Yanga mwishoni mwa Juma hili.
Simba na Yanga zinatarajia kushuka dimbani Oktoba 28 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kuwania pointi tatu zitakazowaweka sawa kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu moja kwa moja kutoka nchini Morocco, Msuva ameanza kwa kuelezea hali yake na maendeleo yake yalivyo ndani ya kikosi cha timu hio mpaka sasa yalivyo.

Msuva amesema kwamba bado wana mechi moja ya kiporo ya Ligi Kuu nchini humo lakini wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mfalme ambapo kesho watajitupa dimbani kuwania tiketi ya kucheza fainali ya kombe hilo.
“Kuna mechi moja ya kiporo bado hatujacheza, tukiicheza hiyo naamini tutakuwa tumejiweka sawa kwenye ligi, kwa sasa tupo kwenye nusu fainali ya Kombe la Mfalme, kesho tunacheza tena” alisema Msuva.
Msuva amefafanua kuwa ligi ya nchini humo si nyepesi hata kidogo kwani imekuwa na ushindani huku akikiri wazi kwamba amejifunza mambo mengi kutoka kwenye ligi hio.
Winga huyo anaamini kwamba pamoja na ugumu wa ligi hio na ushindani uliopo lakini itamfunza mambo mengi yatakayomfanya kuwa bora zaidi.

“Ligi ni ngumu sana, ligi inaushindani mkubwa, nimejifunza mambo mengi naamini itanitengeneza zaidi” alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Msuva amekataa kuelezea chochote kuhusu mchezo wa Simba na Yanga huku akisisitiza kuwa anawahi kwenye mazoezi ya timu yake na kuomba atafutwe siku ya mchezo wenyewe.
“Naomba nipigie siku hio hio, sasa hivi nakwenda kwenye mazoezi” alisema,huo unakua muendelezo wa watu maarufu kukataa kuuzungumzia mchezo huo baada ya msemaji wa wekund wa msimbaji Bwana Haji Manara kusema anafunga mdomo wake mpaka baada ya mpambano huo

0 comments :
Post a Comment