News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 29 October 2017

MAKAMU RAIS WA SIMBA AKIWA HAAMINI ANACHOKIONA MACHONI MWAKE!! UNAHISI NINI KIMEMKWAZA??


Kaimu Makamu Rais wa Simba, Iddi Kajuna alionekana kama haelewi vile kilichokuwa kikitokea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Ilikuwa wakati Simba ikiwavaa watani wake Yanga ambao awali walionekana kuwa “wanapigika” kirahisi lakini mambo yakawa tofauti kabisa.

Pamoja na kuonekana kama Yanga isingekuwa na nafasi ya kushinda, lakini mashambulizi yake mengi yalikuwa ni makali na ya kushitukiza.

Kipa wa Simba, Aishi Manula alikuwa ndiye shujaa wa Simba kutokana na kulazimika kufanya kazi ya ziada takribani mara nne kuikoa timu yake.

Simba ilionyesha soka safi lakini hakukuwa na mashambulizi makali sana kuwa Yanga hofu kama waliyokuwa nayo kabla ya mechi.


Kajuna alikuwa jukwaa kuu akishuhudia mechi hiyo na mara nyingi alikuwa amejishika kichwa kama mtu mwenye majonzi au ambaye haamini kilichokuwa kinaendelea.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment