
Alikuwa mnyama Simba SC aliyekuwa wa kwanza kuwanyangua maelefu ya mashabiki wake vitini kupitia kwa Shiza. Kichuya baada ya kuicheza vyema krosi ya Emanuel Okwi. Hii ilikuwa dakika ya 57 baada ya timu zote kwenda mapumziko zikiwa suluhu bin suluhu.
Dakika tatu baadae Yanga waliweza kusawazisha goli hilo kupitia kwa mshambuliaji wao wa kati Obrey Chirwa na mwisho wa mchezo matokeo kusomeka 1-1.
*TATHIMINI*
Tukianza na wenyeji wa mchezo Yanga SC; waliingia uwanjani wakitumia mfumo wa 4-4-2 . Ukuta wa nyuma ukiwa na walinzi wanne Juma Abdul kulia na Gadiel Mbaga kushoto wakicheza kama walinzi wa pembeni. Kati walisimama Andrew Vicent na nahodha Kelvin Yondani.
Eneo la kati ; Pappy Tshishimbi kama kiungo mkabaji ambaye alikuwa akicheza kama box to box midfielder. Alifanya kazi tatu kwa wakati mmoja , alisimama kama kiungo mkabaji timu ikipoteza mpira , alijenga mashambulizi kati kama kiungo mchezeshaji pia akisogea juu kama kiungo mshambuliaji. Tshishimbi alisimama kati na Rafael Daudi . Kushoto kwao akitaradadi vizuri Geofrey Mwashiuya na kulia Piusi Buswita ambaye jana hakucheza kama winga alisimama kama kiungo mchezeshaji wa pembeni timu ikishambulia pia aliingia kati kukaba.
Mbele walisimama Obrey Chirwa kama mshambuliaji kiongozi kati na Ibrahim Ajibu akicheza kama deep playmaker kujenga daraja la viungo wa kati na safu ya ushambuliaji na wakati huo huo akifanya switching na Chirwa kama mshambuliaji.
Yanga walijipanga vyema kwenye kujilinda wakifanya mashambulizi machache ya kushitukiza lakini yaliyokuwa yamepangwa vyema hususani kipindi cha kwanza . Kama sio umakini wa golikipa wa Simba Aishi Manula kwa mikwaju ya Tshishimbi huenda Yanga wangepata magoli zaidi ya hilo moja .
Tshishimbi aliwatawala Simba eneo la kati atakavyo lakini alikosa sapoti nzuri kwa Rafael Daudi ambaye hakuwa na kasi nzuri kusharabu ubora wa Tshishimbi pale kati . Kushindwa kwa Rafael Daudi kutengeneza kombinesheni nzuri na Tshishimbi kulifanya mara nyingi Ajibu kushuka chini hali iliyoifanya safu ya ushambuliaji ya Yanga kucheza mbali na lango la Simba , kusogea mbele ilihitaji counter na sio kufungua vyumba kwa pasi fupi fupi. Lwandamina kipindi cha pili aliliona hili kwa kumtoa Rafael Daudi na kumwingiza Pato Ngonyani lakini Omog tayari alikuwa amemzidi kete kwa kumuingiza Jonasi Mkude kuondoa utawala wa Tshishimbi eneo la kati baada ya kumzidi vilivyo James Kotei.
Madhaifu ya Yanga yalikuwa kwenye ‘ pre marking ‘ . Hawakuwa wazuri sana kwenye kumkaba mtu asiye na mpira . Zaidi ya mara tano Shiza Kichuya alipokea mpira akiwa huru . Goli lake baada ya krosi ya Emanuel Okwi, hakuwekewa tena ulinzi wa kutosha kabla yakuwa na mpira hali iliyompa uhuru wa kufunga akiwa mbele ya lango la Yanga .
Pia kukosa umakini wa kutumia nafasi za kufunga , dakika ya 82 Emanuel Martin alishindwa kuipatia Yanga SC goli la wazi akiwa yeye na kipa .
Kwa ujumla Yanga wamefunguka lakini kuna nafasi wanakosa watu wenye uwezo mzuri kwa asilimia 100 mathalani kiungo wa kutengeneza kombinesheni na Tshishimbi hususani kwenye offensive patterns. Kama Yanga wangekuwa na Kamusoko ni dhahiri timu isingecheza sana chini kwa maana ya kufunguka zaidi wakitoka box moja kwenda jingine . Pressing kwenye wings haikuwa kubwa kama ilivyozoeleka kwa Saimoni Msuva lakini kizuri Lwandamina amejua kumtumia Buswita kama mchezeshaji kwenye wings pia akivunjikia ndani kusaidia kukaba.
SIMBA SC
Moja ya kitu ambacho Simba watajilaumu leo ni kushindwa kufatilia maendeleo ya Yanga katika mechi zao saba za awali kabla ya leo. Walishindwa pia kuheshimu uwezo wa George Lwandamina katika kusoma wapinzani wake .
Simba waliingia uwanjani na hali ya kujiamini sana kitu ambacho kiliwanyima ‘ command ya mchezo ‘ ( authority ). Walianza na mfumo wa 4-4-2 kama Yanga lakini battling ya Tshishimbi na Kotei pale kati iliwafanya kugeuka na kucheza 4-2-3-1 ili kujaribu kupunguza pressure ya Pappy Kabamba Tshishimbi hali iliyomfanya Haruna kurudi chini kidogo kusaidia kuendesha timu huku Mavugo akibaki kama mshambuliaji pekee mbele ndio maana Simba kipindi cha kwanza walikuwa na possession kubwa lakini hawakuweza kufika langoni kwa Yanga kwa shambulio la maana hata moja .
Kuchagua kumwanzisha James Kotei mbele ya Tshishimbi haukuwa uchaguzi mzuri kutokana na Kotei kutokuwa mzuri sana kwenye battling za kusogeza timu juu katika upinzani mkali . Omog alitakiwa kumwanzisha Jonasi Mkude toka Mwanza akiwa na Mzamiru Yassin au Saidi Ndemla ambaye mara nyingi amekuwa akiamua matokeo katika mechi za watani wa jadi.
Hakutaka kubadilika kwenye mipango yake ya kutumia wing ya kulia kupitia Erasto Nyoni na Shiza Kichuya kushambulia. Ni zaidi ya mechi tatu anatumia mfumo huo kitu ambacho Yanga waliking’amua kwa kutanua kiungo kuziba njia sema walikuwa na makosa kumlinda Shiza Kichuya ambaye alikuwa anafanya switching mara kwa mara ya kuhama kutoka box moja kwenda jingine.
Kizuri kwa Simba SC ni uwezo wa kumiliki mpira , kuwa vyema katika kujenga mashambulizi lakini mipango yao haikuwa mizuri kwenye finishing kutokana na tempo ya mechi .
Goli lao dakika ya 57 ni goli nzuri ambalo lilisukwa vyema toka wing ya kushoto kwa Okwi na kutumia vyema makosa ya walinzi wa Yanga katika kumlinda Kichuya lakini wakashindwa kulinda goli kwa kuruhusu mashambulizi ndani ya 18 yao . Mipango mingi ilikuwa ni kumzibia njia Ibrahim Ajibu lakini wakamsahau Chirwa .
Endapo Simba itashindwa kucheza kwa kasi , kuheshimu uzito wa jezi yao , kuwa na uwezo wa kumsoma mpinzani wake wanaweza kujikuta wanapotea kwenye harakati za ubingwa hususani duru la pili la ligi.
Ukiitazama ni timu ambayo ina makosa machache ya kiufundi hususani nidhamu ya mchezo na jinsi ya kutumia wachezaji waliopo pia kujengeka vyema katika saikolojia ya kusaka ushindi .
By Samuel Samuel

0 comments :
Post a Comment