Akiwa na watoto wake wawili wa kiume, staa wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, ambaye ana umri wa miaka 30 ametangaza kuwa mkewe ni mjamzito.
Messi ambaye ni baba wa watoto wawili, Thiago na Mateo ametangaza hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kufanya tangazo lake hilo lifuatiliwe na watu zaidi ya milioni moja ndani ya saa moja tu.
Huyo utakuwa ni ujauzito wa tatu kwa mke wa Messi ambaye anajulikana kwa jina la Antonella Roccuzzo.
Kauli hiyo inaweza kusababisha mwendelezo wa ushindani kati ya Messi na mpinzani wake wa jadi uwanjani, Cristiano Ronaldo ambaye naye ni baba wa watoto watatu.
Inavyoonekana ni kama wawili hao sasa wamegeuza ushindani wao nje ya uwanja, kwani Ronaldo lipata watoto mapacha hivi karibuni na hivyo kuwa na watoto watatu huku ikidaiwa kuwa mchumba wake ni mjamzito.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA



0 comments :
Post a Comment