News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Friday, 8 September 2017

WENGER AZITILIA SHAKA 4-0 ZA LIVERPOOL ASEMA Alex-Oxlade-Chamberlain ALISHALEGEZWA KABLA YA MECHI


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amechekelea mabadiliko yaliyopitishwa na vilabu vya Premier League kubadili tarehe ya kufunga dirisha la usajili. Kuanzia msimu ujao, dirisha la usajili England litafungwa tarehe, 9 mwezi Agosti kabla msimu mpya haujaanza tofauti na ilivyokuwa likifungwa Agosti 31. Kocha huyo anasema: "Mambo mengi hufanyika sekunde za mwisho ambayo huwa nayajutia. Hii ndiyo maana ninaamini kwamba wakati umefika tubadilishe sheria na tuwe tukifunga soko kabla ya msimu kuanza. "Wachezaji hawajui hatima yao. Wako ndani au nje? Kuna wengine ambao wanachukuliwa na watu alasiri ya mechi, hii ilikuwa inaumiza sana. Huwezi kuwa na wachezaji wanajiandaa kucheza huku kiakili wako nusu ndani na nusu nje."Pia Wenger ametilia shaka kipigo cha 4-0 cha Liverpool akisema  
Alex-Oxlade-Chamberlain aliingia kwenye mechi akiwa akili yake iko kwingine  akasema itakua ni ujinga kuamini eti kwamba Liverpool hawakua wameshasuka dili na mchezaji kuhusu uhamisho kabla ya mechi ile


* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA* Millionaire  Ads
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment