News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday, 21 September 2017

SIMBA WASHINDWA KUITAFUNA MBAO FC: WARUHUSU NYAVU ZAO KUGUSWA WAKITOSHANA NGUVU KWA 2-2

 Tokeo la picha la simba vs mbao fc 2-2
Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Athumani Lazi wa Morogoro, hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na winga machachari, Shiza Ramadhani Kichuya dakika ya 16 akimalizia krosi nzuri ya beki Erasto Edward Nyoni.
Kichuya alishindwa kuendelea na mchezo dakika ya 44 baada ya kuumia na kumpisha Haruna Niyozima, wakati Mbao nalo walimtoa Said Said dakika ya 37 na kumuingza Herbet Lukindo.
Kipindi cha pili Mbao walirudi kwa kasi nzuri na kufanikiwa kusawazisha bao dakika ya 46 tu, kupitia kw3a Habib Kiyombo ambaye hilo linakuwa bao lake la tatu msimu huu.
Hata hivyo, Simba walijibu kwa mashambulizi mfululizo na kufanikiwa kupata bao la pili dakika tatu baadaye, mfungaji kiungo Mghana, James Kotei.   
Mbao hawakukata tamaa, waliendelea kushambulia na kufanikiwa kusawazisha tena dakika ya 81 kupitia Emmanuel Mvuyekire aliyefunga kwa shuti la mbali pia.
Kutoka hapo timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini hakukuwa na mabao zaidi.
Ikumbukwe msimu uliopita, Simba ilishinda mechi zote tatu ilizokutana na Mbao, zikiwemo mbili za Ligi Kuu msimu uliopita Alhamisi ya Oktoba 20 iliposhinda 1-0 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na Jumatatu ya Aprili 10 iliposhindaa 3-2 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo mwingine ulikuwa wa fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup Mei 27, mwaka huu ambao Simba walishinda 2-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Kikosi cha Mbao FC kilikuwa; Kelvin Ingendelezi, Boniphace Maganga, Abubakar Ngalema, Yusuph Mgeta, Yusuph Ndikumana, Sadallah Lipangile, Ibrahim Njohole/Emmanuel Mvuyekire, Hussein Kassanga, Moses Shaaban, Said Said/Herbet Lukindo dk37 na Habibu Kiyombo/Ndaki Kisambale dk62.
Simba: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Method Mwanjali, James Kotei, Nicholaus Gyan/Juma Luizio dk76, Muzamil Yassin, John Bocco, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya/Haruna Niyonzima dk44. 
NAOMBA UTUSAIDIE KU SHERE HABARI KWA KUA FB PAGE YETU INA MATATIZO * USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA* Millionaire  Ads
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment