Baada ya sare ya mabao 2-2, Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amegoma kusalimiana kwa kumpa mkono kocha wa Stoke City, Mark Hughes.
Tukio hilo ambalo lilitokea jana baada ya mchezo huo wa Premier League ambapo Mourinho alionyesha kukasirishwa na matokeo hayo, ambapo baadaye alipoulizwa juu ya tukio hilo akatoa lugha kali.
Mchezo huo umeifanya United kumaliza mbio zake za kushinda mfululizo katika ligi hiyo, hivyo kuwa pointi sawa na Man City, zote zikiwa na pointi 10 katika michezo mine.
Mourinho alitamka: “Siwezi kujibu ujinga, mimi sasa ni mtu mzima, kujibu ujinga ni kupoteza muda, ujinga ujibiwe na wajinga wenyewe.”
Wakati mchezo huo ulipokuwa ukiendelea, Hughes alimsukuma Mourinho, alipulizwa baadaye sababu za kufanya hivyo alisema Mourinho alisogea kwenye eneo lake la kusimama na kutoa maelekezo kwa wachezaji wake

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Millionaire  Ads



0 comments :
Post a Comment