LIPULI imemkatia rufaa mwamuzi, Hans Mabena, kutoka Tanga aliyechezesha mechi Ligi Kuu Tanzania Bara kati yao na Yanga, iliyochezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Klabu hiyo imewasilisha rufaa hiyo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikipiga kadi nyekundu aliyoonyeshwa beki wao, Asante Kwasi, kutokana na kumchezea rafu kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi.
Kwasi alionyeshwa kadi hiyo baada ya kupewa kadi mbili za njano.
Kocha wa Lipuli, Seleman Matola, ameuthibitishia uongozi wa klabu hiyo kuwasilisha rufaa hiyo, baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.
Matola alisema wanasubiri majibu ya rufaa hiyo, kwani anaamini haki itatendeka dhidi yao.
Katika mechi hiyo, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 huku Kwasi akishindwa kumaliza dakika 90, baada ya kulimwa kadi hiyo
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*

0 comments :
Post a Comment