News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Friday, 1 September 2017

KAULI YA DAUDA JUU YA SIMBA ILIYOMPONZA MTANDAONI YATOLEWA TENA NA JULIO


KOCHA wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio,’ amesema Simba wasijiamini kupita kiasi na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba waliibuka na ushindi huo katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ambao walianza msimu mpya kwa kuchukua Ngao ya Jamii.
Wekundu wa Msimbazi hao walifanikiwa kuwafunga Yanga kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 5-4 katika mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, baada ya kutoka sare tasa ndani ya dakika 90, iliyochezwa Agosti 23, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo, Julio ameitahadharisha Simba kutojiamini kupita kiasi, kwani bado wana safari ndefu ya kufanikisha malengo yao ya kuwania ubingwa kauli kama hii aliioa mchambuzi Nguli wa maswala ya soka nchini na mtangazaji wa kipindi cha michezo Redio moja hapa nchini Shafii Dauda kwamba Simba isijiamini sana kwa mwanzo huu lakini ilipokelewa tofauti na kushambuliwa kila kona kwenye mtandao yakionekana kua ni majungu lakini leo hii imetolewa na mtu mwenye heshima yake Ndani na nje ya klabu ya simba Julio ameshawahi kuifundisha simba kwa mafanikio

Julio alisema Simba wasifikirie ubingwa kwa sasa kutokana na matokeo waliyoyapata katika mechi ya Ngao ya Jamii na ile ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
Alisema kitendo cha mashabiki na baadhi ya viongozi kuanza kufikiria watachukua ubingwa wa msimu huu ni mapema sana, kwani wanatakiwa kupambania ushindi kwa kila mechi.
“Watu watakaokwambia Simba bingwa msimu huu watakuwa hawajui mpira, kwani ni mapema kujihakikishia sasa hilo, lakini ni vizuri wakakumbuka ilivyoanza msimu uliopita.
“Kama watakuwa na kumbukumbu, Simba ilianza vizuri kwa matokeo ya ushindi, lakini katikati ya ligi ikaanza kupoteza makali na kujikuta wakimaliza nafasi ya pili,” alisema Julio.
Simba wanatarajia kucheza na Azam katika mechi itakayochezwa Jumatano ijayo, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment