News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday, 18 September 2017

KAMA HUJUI BASI NDIO HIVYOO!! OKWI PEKEE ANA MAGOLI MENGI KULIKO "TIMU ZOTE" LIGI KUU KASORO SIMBA TU


Straika Emmanuel Okwi amefunga magoli mengi kuliko timu yoyote kwenye Ligi Kuu, ukiondoa timu yake ya Simba.
Okwi aliyefunga magoli mawili kwenye mechi ya Jumapili iliyopita dhidi ya Mwadui na kuifanya timu yake ishinde mabao 3-0, amefikisha idadi hiyo ya magoli baada ya kufunga magoli manne kwenye mechi ya ufunguzi, Simba ikiikandika Ruvu Shooting mabao 7-0.
Ukiondoa Simba, hakuna timu yoyote kati ya 15 zilizosalia zilizofisha idadi ya magoli ya straika huyo.
Timu yenye magoli mengi ya kufunga ukiondoa Simba iliyofikisha magoli 10 ni Mtibwa Sugar ambayo inayoongoza Ligi Kuu kwa pointi tisa, yenye magoli manne tu.

 * USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA* Millionaire  Ads
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment