News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday, 7 September 2017

JUUKO MURSHID NA OKWI KUINGIA USIKU HUU TAYARI KWA MPAMBANO NA AZAM

Tokeo la picha la Emmanuel Okwi na Juuko Murshid
Mastaa wa Simba Emmanuel Okwi na Juuko Murshid waliokuwa wakiitimukia timu yao ya taifa ya Uganda wanatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam usiku huu na kujiunga na wenzao kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Azam.
Simba wanatarajiwa kukipiga na wapinzani wao hao katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Azam Complex maarufu kwa jina la Uwanja wa Chamazi uliopo Dar es Salaam.
Taarifa kutoka Simba zinaeleza kuwa wachezaji hao walikosa mazoezi ya leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Uhuru lakini wtawasili muda wowte usiku huu.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amekiri juu ya ujio wa wachezaji hao.
Viingilio katika mchezo huo wa Chamazi utakaoanza Saa 1:00 usiku vitakuwa ni Sh. 10,000 kwa jukwaa la VIP na 7,000 kwa mzunguko
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA* Millionaire  Ads
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment