
HARUNA Nyonzima alikuwa majeruhi wakati alipofanyiwa rafu mbaya na mchezaji wa Ruvu Shooting katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya soka Tanzania bara. Mashabiki wa Simba wakawa na wasiwasi kuhusu maendeleo ya fundi huyo uwanjani. Lakini sasa imebainika kwamba Nyonzima yuko fiti na amejiandaa kikamilifu kuwavaa Azam FC Jumamosi. "Haruna amepona kabisa, han
a tatizo lolote na anajiandaa tu kwa mechi dhidi ya Azam na mechi nyingine zinazokuja,’’ amesema mmoja kati ya viongozi wa Simba. Amesema kama hatakuwa na shida nyingine yoyote ataiongoza Simba kwenye mechi hiyo ngumu dhidi ya Azam na kutokana na mfumo wa sasa wa kocha Joseph Omog, anaweza kusimama kama kiungo mshambuliaji wa pembeni. Omog ni kocha anayevutiwa na wachezaji wenye kasi aina ya Haruna na tangu asajiliwe Simba amekuwa akipenda sana kumtumia kama winga wa kushoto badala ya nafasi ya kiungo wa kati kama alivyokuwa anacheza Yanga. ‘"Unajuwa Omog anajua kwamba Haruna ana vitu vingi uwanjani , na kwakuwa simba inaviungo wengi wa kati, Haruna anaweza kuwa anapishana na Shiza Kichuya pembeni mwa uwanja, halafu Said Ndemla na Muzamiru Yasini wakasimama katikati," amesema mtoa habari huyo. Omog katika mazoezi yanavyoendelea anatengeneza namna ambayo James Kotei na Jonas Mkude wanaweza kuanza kwa pamoja, hatua ambayo inakusudia kusuka kiungo cha kukaba imara zaidi, wakati Method Mwanjali na Salim Mbonde wakisimama kama mabeki wa kati, huku Erasto Nyoni na Ali Shomari wakitarajiwa kuanza pembeni. Omog anataka kuendelea kuwapumzisha Mohammed Hussein “Tishabalala” na Shomari Kapombe wawe katika utimamu wa asilimia mia kabla ya kuingia kwenye mikiki ya Ligi Kuu.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*

0 comments :
Post a Comment