YANGA
KOCHA Mkuu wa timu ya Njombe Mji, Hassan Banyai baada ya kupoteza dhidi ya Prisons kwa bao 2-1 ameibuka na kusema kuwa licha ya kuwaheshimu Yanga kama timu kongwe lakini hawatakubali kupoteza dhidi yao.Akizungumza na Saleh Jembe, Banyai amesema wanajua kama michezo ya ligi kuu ni migumu lakini hatakubali kupoteza tena dhidi ya Yanga japo ni timu kubwa na wanaiheshimu.
“Tunajua kuwa Yanga ni timu kubwa na tunaiheshimu lakini niwaambie tu watatusamehe kwani hatutokubali kupoteza kwa mara ya pili licha ya ligi kuu bara kuwa na michezo migumu kwani kila timu wanataka ushindi hili waweze kusonga mbele,” alisema Banyai.
SIMBA
MLINZI wa kushoto wa Simba na Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ maarfufu Zaidi Tshabalala amefungukwa kuwa mchezo wao wa wikiendi hii mbele ya Azam utakuwa mwepesi kwao kuibuka na pointi tatu kutokana na malengo ya kupata pointi mbele ya timu yoyote ile waliyojiwekea.Simba wanatarajiwa kuwa wageni wa Azam kwenye pambano la ligi kuu ambalo litapigwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar, ambapo mchezo baina ya vikosi hivi viwili utakuwa wa kwanza kupigwa katika uwanja huo.
Akizungumza Tshabalala amesema kuwa licha yakutambua ugumu waliokuwa nao Azam lakini jambo hilo haliwazuii wao kuibuka na pointi kama ambavyo wamepania kufanya hivyo kwenye kila mchezo wao ambao wataucheza msimu huu.
“Azam wagumu kwa wengine lakini kwetu watalainika tu kwa sababu hii siyo mara ya kwanza tunakutana nao na tunawajua vizuri jinsi ambavyo wamekuwa wakicheza, kwamba tutumie mbinu gani kupata pointi na kizuri zaidi ni kwamba tumekusanya nyota wao ambao walikuwa tishio kwetu kwenye misimu kadhaa nyuma.
“Unajua nina uhakika mkubwa wa kushinda mechi hiyo kwa sababu ya malengo yetu ya mwaka huu ya kupata pointi haijalishi tunacheza na mpinzani gani awe mdogo au mkubwa, kitu cha muhimu na kwanza ni kushinda na kupata pointi na siyo jambo lingine lolote lile,” alisema Tshabalala.
MLINZI wa kushoto wa Simba na Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ maarfufu Zaidi Tshabalala amefungukwa kuwa mchezo wao wa wikiendi hii mbele ya Azam utakuwa mwepesi kwao kuibuka na pointi tatu kutokana na malengo ya kupata pointi mbele ya timu yoyote ile waliyojiwekea.
Simba wanatarajiwa kuwa wageni wa Azam kwenye pambano la ligi kuu ambalo litapigwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar, ambapo mchezo baina ya vikosi hivi viwili utakuwa wa kwanza kupigwa katika uwanja huo.
Akizungumza Tshabalala amesema kuwa licha yakutambua ugumu waliokuwa nao Azam lakini jambo hilo haliwazuii wao kuibuka na pointi kama ambavyo wamepania kufanya hivyo kwenye kila mchezo wao ambao wataucheza msimu huu.
“Azam wagumu kwa wengine lakini kwetu watalainika tu kwa sababu hii siyo mara ya kwanza tunakutana nao na tunawajua vizuri jinsi ambavyo wamekuwa wakicheza, kwamba tutumie mbinu gani kupata pointi na kizuri zaidi ni kwamba tumekusanya nyota wao ambao walikuwa tishio kwetu kwenye misimu kadhaa nyuma.
“Unajua nina uhakika mkubwa wa kushinda mechi hiyo kwa sababu ya malengo yetu ya mwaka huu ya kupata pointi haijalishi tunacheza na mpinzani gani awe mdogo au mkubwa, kitu cha muhimu na kwanza ni kushinda na kupata pointi na siyo jambo lingine lolote lile,” alisema Tshabalala.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*

0 comments :
Post a Comment