News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday, 2 September 2017

HABARI KUBWA ZA SIMBA ASUBUHI HII NIMEKUWEKEA HAPA ZOTEE USHINDWE WEWE TU!!

MGHANA WA SIMBA FASTAAAA!! KWA AJILI  YA AZAM

Mshambuliaji mpya wa Simba, Nicholaus Gyan anatarajia kutua nchini leo hii tayari kwa kuungana na wenzake kisha
kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu bara dhidi ya Azam FC.

Gyan ambaye mwanzoni mwa mwezi ulipotia alitua nchini kwa ajili ya kumalizana na Simba kisha kutambulishwa katika Tamasha la Simba Day alirudi kwao Ghana kumalizana na timu yake aliyokuwa akiitumikia.

Kocha wa Simba, Joseph Omog ameshusha pumzi baada ya kupewa taarifa za kurejea nchini kwa Gyan ambaye ataiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji ambayo hadi sasa ina mabao saba.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Omog alisema: “Kama atatua kweli kesho (leo) ni jambo zuri kwetu kwani ataiongezea nguvu safu yetu ya
ushambuliaji kwa ajili ya kukabiliana na Azam.

“Gyan yupo vizuri aliyonyesha uwezo mkubwa tulipocheza na Rayon Sports (ya Rwanda katika Simba Day) kwa hiyo ni matumaini yangu atatusaidia katika mechi hiyo na nyingine zinazokuja.”

"OKWIIIII"  JAMAA AMESEMA ATAFUNGA SANA MSIMU HUUU YANI SANAAA!!

MUDA mfupi tu baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Misri na kuiwezesha Uganda kukaa kileleni mwa Kundi E la kufuzu Kombe la Dunia 2018, Emmanuel Okwi amesema atafunga sana msimu huu.

Siku sita baada ya kuifungia Simba mabao manne katika ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika Ligi Kuu Bara, Okwi ameifungia Uganda ‘The Cranes’ bao pekee lililoipa ushindi wa 1-0 dhidi ya Misri.

Okwi ameifunga Misri yenye nyota kadhaa wakiwemo Mohamed Salah wa Liverpool na Mohamed Elneny wa Arsenal, ambao licha ya kupambana hawakuweza kuisaidia timu yao kusawazisha.
Akizungumza kutoka Uganda, muda mfupi baada ya mechi dhidi ya Misri, Okwi aliliambia Championi Jumamosi kuwa, amepania kufunga mabao mengi msimu huu na atapambana kuweza kufunga muda wote.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Okwi amebainisha kuwa, kutokana na Mungu kuendelea kumuangazia neema ya mabao, atajitahidi kuuwasha moto katika kila mchezo atakaocheza lengo likiwa ni kulinda jina lake.
“Naendelea kumuomba Mungu ili tu asinitupe, nataka anipe afya njema ili niweze kucheza kila mechi na kufunga mabao niwezavyo.

“Mashabiki wengi wanatarajia kuona nafanya nini nikiwa uwanjani, ndiyo maana nasema naomba Mungu anisaidie niwe nafunga kila siku ili nilinde jina langu.
“Kiukweli ninapokuwa kikosini hasa Simba, sipo tayari kuona timu yangu inakosa matokeo mazuri, nimekuwa nikitamani sana kufunga na kweli inakuwa hivyo, najua mashabiki wanahitaji matokeo mazuri.

“Nasema kutoka moyoni kwamba, bado nitafunga na nitafunga kadiri ninavyopata nafasi uwanjani, Simba hii ya sasa imekamilika kila idara na sidhani kama tutakosa ubingwa msimu huu,” alisema Okwi.

Akizungumzia mechi ya Uganda na Misri, Okwi alisema: “Ilikuwa mechi nzuri kwetu, tulipambana na kupata ushindi na itakuwa furaha kwangu nikiona tunacheza Kombe la Dunia.”
Katika mchezo huo wa juzi ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Mandela jijini Kampala, Uganda, Okwi alifunga bao lake dakika ya 51.

Uganda inaongoza Kundi G ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Misri yenye pointi sita huku timu zote zikiwa zimecheza mechi tatu. Timu nyingine za kundi hilo ni Ghana na Congo.
Timu hizo zitarudiana Jumanne ijayo nchini Misri.

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment