YANGA 1-1 LIPULI 'LIVE' FULL TIME, UWANJA WA UHURU
FULL TIME
Dk ya 94: Mwamuzi anamaliza mchezo, matokeo ni 1-1.
Dk ya 93: Asante Kwasi wa Lipuli anapewa kadi nyekundu, mwamuzi wa kati alijadiliana na mwenzake wa pembeni na kutoa kadi ya pili ya njano kwa mchezaji huyo.
Dk ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 4 za nyongeza.
Dk ya 89: Yanga wanaonekana kutokata tamaa wanafika langoni lakini bado mambo magumu
Dk ya 84: Tshishimbi anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo, analalamika lakini mwamuzi anapa kadi hiyo.
Dk ya 79: Lipuli wanarudi nyuma, muda mwingi mpira unachezwa kwenye nusu yao.
Dk ya 78: Yanga wanafanya mashambulizi lakini bado mambo magumu.
Dk ya 70: Yusuph Mhilu wa Yanga anaingiam anatoka Emmanuel Martine.
Dk ya 69: Mchezo unaendelea, wachezaji wa timu zote wanatumia nguvu kubwa kupambana.
Dk ya 65: Tshishimbi anachezewa faulo mguuni, mchezo unasimama anatabiwa.
Dk ya 60: Ngalema na Ajibu wanatifuana lakini mwamuzi anapuliza filimbi.
Dk ya 57; Yanga wanafika langoni mwa Lipuli lakini wanashindwa kutumia nafasi.
Dk ya 50: Mashambulizi ya zamu kwa timu zote.Mchezo umeanza kwa kasi.
Kipindi cha pili kimeanza.
Mapumziko
Wachezaji wa Lipuli wanalalamika kuwa mpira ulikuwa haijaingia baada ya Ngoma kuupiga kichwa, lakini mwamuzi anaweka kati.
Dk ya 45: GOOOOOOOOOOOOOOO!!! Yanga wanasawazisha kupitia kwa Ndoma lakini utata unatokea.
Lipuli wanapata bao kupitia kwa Seif Abdallah ambaye akicheza vizuri kwa kuwatoka walinzi wa Yanga kabla ya kufunga.
Dk ya 44: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!
Dk ya 43: Ngoma anaingia na mpira lakini anazuiliwa.Dk ya 42: Ksi ya mchezo imebalansi kwa timu zote.
Dk ya 38: Mchezo unaendelea.
Dk ya 36: Yanga wanapata kona, inapigwa kipa wa Lipuli anachezewa fau, mchezo unasimama kw amuda anatibiwa.
Dk ya 31: Yanga wanapata kona, inapigwa na Juma Abdul, inaokolewa na kuwa kona nyingine.
Dk ya 27: Yanga wanapata nafasi ya kufunga kupitia Raphael Daudi lakini anashindwa kutumia vizuri nafasi.
Dk ya 22: Yanga wanapata kona ya pili lakini inaokolewa.
Dk ya 20: Lipuli wanafanya shambulizi kali, mpira wa kichwa ulipigwa na Seif unapaa juu ya lango baada ya kuwatoka walinzi.
Dk ya 17: Yanga wanapata kona, inapigwa lakini inaokolewa, kunatokea vuta nikuvute kati ya beki wa Lipuli, Novalty Lufunga na straika wa Yanga, Donald Ngoma.
Dk ya 16: Yanga wameanza kupiga pasi nyingi za kuelewana.
Dk ya 14: Lipuli bado wanaonekana kuwa imara na kutowaruhusu Yanga kucheza soka la kuutawala mchezo.
Dk ya 11: Lipuili wanafika langoni mwa Yanga lakini mpira unapaa juu ya lango.
Dk 8: Tshishimbi na Ngoma wanacheza pasi nzuri lakini mpira unatoka.
Dk ya 5: Yanga wanamiliki mpira muda mwingi.Dk ya 1: Mchezo umeanza kwa kasi ndogo.
Kipindi cha kwanza kimeanza, huu ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu zote zimeingia uwanjani kucheza mchezo wao wa kwanza msimu wa 2017/18.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment