News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 13 August 2017

WENGER AMWAGA POVU: GIROUD HAUZWI KWA HELA YEYOTE NA MWENYEWE KASEMA HAENDI KOKOTE KWA HIO MWACHENI


London, England

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amewaambia wanaomtaka mshambuliaji wa timu hiyo, Olivier Giroud kuwa hauzwi.

Arsenal wamekuwa wakitajwa mara kwa mara kuwa wanaweza kumuuza mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa, lakini kocha huyo amesema kuwa mchezaji huyo hawezi kuuzwa kwa sasa.

Klabu ya Everton, imetenga kitita cha pauni milioni 20 zaidi ya shilingi bilioni 50, kwa ajili ya mshambuliaji huyo ambaye aliifungia Arsenal bao la ushindi kwenye matokeo ya 4-3 waliyoyapata dhidi ya Leicester City kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi wikiendi iliyopita.

“Ni vigumu kumfanya kila mshambuliaji awe na furaha klabuni kwako, lakini tuna michuano mingi na naamini kila mmoja anaweza kupata nafasi ya kucheza.

 “Nampenda mshambuliaji wangu, Olvier Giroud, amesema hataki kuondoka nami nafurahi sana kusikia hivyo.


 “Nilikuwa nimefungua mlango kwake kwa kuwa nilijua kuwa ninawashambuliaji wengi lakini amesema hataki kuondoka nami nimefurahia jambo hilo, hivyo ni vizuri ieleweke kuwa hauzwi,” alisema Wenger.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment