News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 13 August 2017

WAHENGA CHELSEA WAPIGWA MIGUU YA BAJAJI 3-2 HUKU CAHIL NA FABREGAS WAKILAMBWA UMEME "KADI NYEKUNDU'



Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea wameanza vibaya msimu mpya baada ya kuchapwa kwa mabao 3-2 wakiwa nyumbani Stamford Bridge jijini London.

Chelsea wamefungwa na Burnley katika mchezo uliotawaliwa na vituko vya kila aina.

Hadi mapumziko Chelsea ilikuwa nyuma kwa mabao 3-0 huku ikiwa imempoteza beki wake Garry Cahill.



Kipindi cha pili Alvaro Morata alijitahidi kufunga bao moja, lakini dakika chache baadaye kiungo mkongwe Cesc Fabregas akalambwa kadi ya pili ya njano na kuzaa nyekundu.

Wakiendelea kucheza pungufu, Chelsea walipata bao la pili lililofungwa na beki David Luiz na ndiyo ukawa mwisho uliozaa matokeo ya mabao 3-2.





Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment