News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Tuesday, 15 August 2017

UONGOZI TFF HATA HAUJAANZA KAZI RASMI HAJI MANARA AWAWASHIA MOTO SOMA HAPA ALICHOWAAMBIA!!


RAIS mpya wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Wallace Karia na Makamu wake, Michael Wambura, bado hawajaanza kuchanganya kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi za shirikisho hilo, lakini Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameamua kuwawahi mapema na kuwauma sikio.
Manara amesema akina Karia ni lazima wajue Watanzania walikuwa wanakwazwa na kitu gani, kisha kuweka mambo sawa na kuhakikisha soka linachezwa kwa haki kwa kila timu.
“Unajua TFF, iligeuka kichaka, hivyo viongozi wapya watambue fika Watanzania wameamka na wanataka haki ili soka lisonge mbele, vipaji vipo mikakati ndiyo inatakiwa ya kutufikisha mbali,” alisema.
Manara alisema Karia amepita kwa kishindo hiyo ni ishara ya kujua Watanzania wanahitaji awavushe hatua moja kwenda nyingine na kwamba ana mpango mzuri hasa uwazi wa mapato na matumizi.
“Kikubwa ni atimize kile ambacho alikiahidi kwani mikakati yake ni wazi kwamba analitakiwa soka lisonge mbele,”alisema.
Karia amesema moja ya atakayoyafanya ni kuboresha kamati ndani ya shirikisho hilo huku akiahidi matumizi na mapato ya TFF yatawekwa wazi. 

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment