THIERRY HENRY ASEMA ARSENAL HAITAZAMIKI NA HAISTAHILI KUTAZAMWA
NYOTA wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry, ameonekana kukerwa na kiwango kilichooneshwa na Gunners katika mchezo wao wa juzi ambao waliambulia kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Liverpool na ameamua kuipa jina kama timu ambayo haifai kuangaliwa mechi zake. Katika mchezo huo wa juzi kikosi hicho cha Arsene Wenger kilionekana kufa kabisa kwenye safu ya kiungo wa kati hali ambayo iliwapa nafasi Liverpool kutakata kwa kutumia mashambulizi ya kushtukiza yaliyowafanya waondoke kifua mbele kwenye dimba lao la Anfield. Walikuwa ni wachezaji, Roberto Firmino na Daniel Sturridge, waliokuwa wakitamba katika eneo la hatari na huku Sadio Mane na Mohamed Salah nao wakionekana kutamba kwa kukimbia na mpira kutoka upande mmoja hadi mwingine kutokana na kukosekana mtu wakuwadhibiti. Kutokana na hali hiyo, Henry alisema juzi kwamba hawezi kuendelea kuzitazama mechi za timu yake hiyo ya zamani baada ya kushuhudia jinsi ilivyopasuliwa na vijana hao wa Jurgen Klopp. "Hii ni timu ambayo haistahili kuangaliwa. Ilifika wakati fulani nilitaka kuondoka uwanjani. Ni vigumu kuvumilia," alisema Henry katika mahojiano na Sky Sports. "Sijafurahishwa na timu na sidhani kama mashabiki wote hawapo hivyo. Hili ni tatizo. Arsenal kulikuwapo na utulivu na hii si presha ambayo mtu unatakiwa kuwa nayo kwenye klabu kubwa kama hii,” aliongeza Mfaransa huyo.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment