News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Tuesday, 29 August 2017

SAKATA LA BUSWITA LACHUKUA SURA MPYA: MBAO WAKIRI NI MCHEZAJI HALALI WA .....




Siku chache baada ya kutoka taarifa kuwa kiungo mshambuliaji Pius Buswita amefungiwa na Shirikiso la Soka la Tanzania (TFF) kutokana na kusaini mkataba wa kujiunga na timu mbili katika msimu mmoja, Yanga wameibuka na kulifafanua hilo.
Buswita alijiunga na Yanga miezi kadhaa iliyopita wakati wa dirisha kubwa la usajili lililopita, lakini kulikuwa na taarifa kuwa pia alikuwa amesajiliwa na Simba akitokea kwenye timu yake ya Mbao FC ya Mwanza.
Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema hadi kufikia asubuhi ya leo Jumanne walikuwa hawajapata barua ya adhabu hiyo zaidi wanasikia kwenye vyombo vya habari.  
Nyika amesema kuwa wao wanatambua kuwa mchezaji huyo ni mali yao lakini kinachotangazwa ni figisu, hivyo wanasubiri barua kupata uhakika wa hicho kinachosemwa kisha watakuwa na kitu cha kuzungumza.
Aliongeza kuwa wao walifuata taratibu zote za uhamisho wa mchezaji huo ikiwemo kupata barua kutoka Mbao FC kumruhusu mchezaji huyo kusajiliwa na Yanga.
Naye Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema hawezi kufafanua zaidi kuhusu Buswita kwa kuwa siyo mchezaji wao ni mali ya Yanga na wao walimruhusu kuondoka kwenda Yanga.
Amesema mkataba wao na Buswita ulimalizika, hivyo alikuwa huru kwenda kwenye timu anayoita, amesisitiza kuwa wanaotakiwa kulizungumzia suala hilo ni Yanga kwa kuwa wao ndiyo wanaommiliki mchezaji huyo.

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment