Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage ametoa ushauri kwa wapinzani wao wa jadi Yanga kuelekea mchezo wa Agosti 23 katika Ngao ya Jamii, mchezo ambao utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana kwenye mchezo huo ikiwa ni matayarisho ya msimu ujao wa 2017/18, ambapo timu zote zipo kwenye visiwa vya Zanzibar zikijiandaa kwa mchezo huo.
Akizungumza zaidi Rage kuhusu mchezo huo amesema:
“Namhurumia sana mpinzani wangu wa jadi, mimi ningekuwa kiongozi wa Yanga, tarehe 23 ningesema hiyo Ngao ya Hisani basi chukueni tu.
“Maana kila nikiangalia pale Yanga wa kumzuia Okwi simuoni, wa kumzuia Bocco sioni, sasa Niyonzima zile majalo zake zile anazotupa, zinaleta raha ya ajabu.
“Mimi nina uhakika Agosti 23, Yanga akipona sana kala saba, hapo ni kama wamepata bahati, sasa sijui wanaenda Pemba kufanya nini, labda wanaenda kuchuma karafuu.
“Unakuja kukutana na Simba ambaye amejeruhiwa, sisi hatujapata ubingwa muda mrefu, yaani Simba aliyejeruhiwa, akikukuta njiani…ebwana hatari kubwa.”
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment