Asubuhi ya leo ndio lile pambana la ndondi lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa kati ya bondia Floyd Money Mayweather na bingwa wa UFC Conor McGregor ilimepigwa.
McGregor alifanikiwa kwenda hadi katika raundi ya 9 lakini ilipofika raundi ya 10 mambo yalibadilika baada ya Mayweather kumshambulia sana hadi Gregor aliyekuwa hoi sana huku ikiwa imebaki dakika 1:55 kwa pambano kuisha
Ushindi wa asubuhi ya leo umezidi kumpa rekodi nzuri Mayweather ambapo sasa Mmarekani huyo anakuwa amecheza mapambano 50 ya mashindano bila kupigwa.
McGregor alitabiriwa kupigwa kabla hata ya mchezo huu kutokana na uzoefu wa Mayweather katika mchezo wa boxing na alionekana kuzidiwa kweli dakika za lala salama za pambano hilo na Mayweather akatumia mwanya huo kumuangusha.
Katika raundi ya 1 na ya 2 hadi 3 McGregor alionekana alionekana kummudu Mayweather huku refa akamuonya kutokana na aina ya upigaji wake ambapo alionekana kumpiga Mayweather chini ya kichwa.
Baada ya raundi ya 4 kuisha na Gregor kuonekana mchangamfu, kibao kilianza kubadilika raundi ya 5 ambapo alianza kuonekana kuchoka na ilipofila ya 8 McGregor alionekana hoi zaidi ndipo ya 10 alishambuliwa sana akiwa hoi bina taaban.
Baada ya mchezo huo Floyd alisema “nimewapa mashabiki kile walichotaka kukiona, baada ya mpambano ya Pacquao niliwaahidi kwamba nitarudi kuwafurahisha na leo wameona nilichofanya” alisema Mayweather huku akisisitiza “ni mpambano wangu wa mwisho.”
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment