Kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Haruna Niyonzima alijua usiku wa kuamkia jana kwa ajili ya kuungana na wenzake kwenda kambini kujiandaa na Tamasha la Simba Day litakalofanyika kesho Jumanne.
Niyonzima ambaye alikuwa Yanga, alitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, ambapo alipokelewa na Kaimu Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Iddi Kajuna na kuondoka naye.
Niyonzima alikuwa na familia yake wakati akiwasili ambapo alipelekwa kwenye nyumba aliyopangiwa na klabu hiyo baada ya awali kuondoka na kila kitu vingine akauza alipomalizana na Yanga.
Simba inatarajiwa kucheza dhidi ya Rayon Sport katika tamasha hilo litakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.


0 comments :
Post a Comment